Habari

Don Jazzy awamwagia hela ‘wafuasi’ wake wa Twitter


Producer wa Mavin records Michael ‘Don Jazzy’ Collins Ajereh, wiki iliyopita aliamua kuwamwagia hela baadhi ya followers wake kwenye mtandao wa Twitter kwa kuwaomba akaunti zao za benki baada ya wao kulalamika kuwa wako ‘broke’.
Muda mfupi tu baadaye, wafuasi watano waliopokea ujumbe kutoka kwenye benki zao kuwa ‘mshiko’ umeshaingia walitweet kumshukuru kwa kuwavusha tutani.
Don Jazzy alisema, “I do not want this to be perceived as a public relations stunt. Napenda kufanya mambo yangu kimya kimya. Nimeshawahi kugawa hela kabla, lakini kwakuwa hii ilikuwa kwenye timeline basi imejulikana. Imetokea tu kuwa miongoni mwao wameniomba hela. Imetokea muda huo na wala sikupanga. Wengine wengi wameomba ushauri, record deals na mambo mengine tofauti,najaribu tu kufanya kile nachoweza.”
Miongoni mwa waliofaidika na mgao huo Mr. Adeyemi, alidai kuwa amepokea N100, 000 (zaidi ya shilingi milioni moja za Tanzania) kutoka kwa producer huyo.
Mwingine aitwaye @tweetlawunmi, alionesha shukrani zake kwa kupokea pesa akisema, “Thank You. Thank you! Thank You! God bless you abundantly.”
Ingawa wengine wanasema anafanya hivyo kujipatia umaarufu,Jazzy anasema anajaribu tu kuwafanya mashabiki wake watabasamu.
Mwezi uliopita producer huyo pia aligawa namba za vocha kwaajili ya muda wa maongezi wa simu zenye thamani zaidi ya lakini tatu kupitia Twitter.
Don Jazzy anajulikana sana kwa kazi alizomtengenezea D’Banj na ambazo zimemfikisha hapo alipo japo urafiki na ubia wao ulivunjika miezi ya hivi karibuni na kusababisha kufa kwa label ya Mo’Hits iliyokuwa inamilikiwa na wote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents