HabariMichezo

Dubai kufanya Tamasha kubwa la mashabiki wa FIFA

Dubai inategemewa kuhodhi moja kati ya matamasha sita ya mashabiki wa fifa (FIFA FAN FESTIVALS). Tamasha hili la kutazama kombe la dunia linategemewa kuwa na eneo la kutazama mubashara mechi za kombe la dunia katika eneo la heshima la Vista maeneo ya Dubai harbor, eneo lenye uwezo wa kuchukua mashabiki 10,000 kwa siku.

Kila dakika,kila saa ya mpira wa kombe la dunia mwaka huu utaoneshwa mubashara kupitia runinga kubwa zilizotengezwa zenye ukubwa wa mita mraba (square meters) 330, zenye uwezo wa sauti wa 4D.
Kupitia tamasha hili, mashabiki wanategemewa kujihisi kama wapo uwanjani na wataweza kusherehekea kwa pamoja na wengine wote wanaotazama duniani kote. Tamasha hili linalofahamika kwa jina la BUd x FIFA Fan Festival litakua na burudani za Dj katika na mwisho wa mechi, watumbuizaji pamoja na michezo mbali mbali bila ya kusahau vyakula vya kila aina na teknolojia kubwa za kuonesha anga na mengineyo.
Tamasha hili limedhaminiwa na kampuni ya Budweiser na mshirika rasmi ni kampuni kubwa ya viatu na mavazi ya Adidas pamoja na Dubai Harbor.
Linategemewa kuanza tarehe 20 Novemba mpaka 18 Disemba.

 

Katika kurahisisha usafiri wakati wa kombe la dunia, umoja wa falme za kiarabu UAE wametoa ofa ya Multiple entry Visa inayokuruhusu kuingia na kutoka zaidi ya mara moja kwa wale wenye kadi maalumu ya Hayya kwa siku 90 ambayo itagharimu kiasi cha shilingi 63,000 Tzs tu.
Akizungumza CEO wa Dubai Festivals and Retail Establishment (DFRE) amesema “Dubai inayo furaha kuchaguliwa kuwa moja kati miji sita iliyochaguliwa duniani kujodhi FIFA Fan Festival na tunakaribisha mashabiki wote duniani kuhudhuria”

Kwa taarifa zaidi, unaweza kutembelea www.budxfifadubai.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents