Michezo

Edo Kumwembe atoa ya Moyoni kinachoendelea Simba

Nilimuona Kelvin Yondani akiwa na kitambaa cha unahodha wa timu yake Geita Gold. Ilikuwa siku chache zilizopita. Nikakimbilia katika mtandao wa Wikipedia kutazama umri wake.

Msela Kevin yupo uwanjani mpaka leo. Nadhani hata msimu ujao atakuwepo uwanjani. Jina? Kelvin Yondani. Tarehe ya kuzaliwa? Oktoba 9, 1984. Umri? Miaka 39. Bado Kelvin anadunda katika nafasi ngumu ya ulinzi wa kati. Akiwa katika umri huu amekumbana na kina Fiston Mayele, Prince Dube, Jean Baleke na wengineo.

Kelvin Yondani akiwa na Juma Nyosso

Kwa mujibu wa mtandao huo huo wa Wikipedia inaonyesha kwamba John Bocco ambaye jina lake lipo katika usajili wa Simba msimu huu ana umri wa miaka 34. Amepitwa miaka mitano na Yondani. Kwanini Bocco hayupo uwanjani? Kwa sasa nasikia anasomea ukocha huku akifundisha timu ya Simba chini ya umri wa miaka 17. Ni baada ya kumfukuza na kumwambia amezeeka katika soka letu.

John Bocco

Ni kitu ambacho tumekuwa tukifanya mara nyingi baada ya kumchoka mchezaji. Mchezaji mwenye roho ndogo huwa anakimbia akiambiwa hivi. Sana sana kama anacheza Simba au Yanga. Huwa anaukubali uzee, anavunjika moyo, kisaikolojia anajiona mzee kweli.

Inatokea sana kwa wachezaji wazawa. Wachache ndio wanaweza kuwa wabishi. Ni kama inavyotokea kwa Yondani.

Kelvin Yondani

Mpaka leo nina uhakika kwamba Bocco angeweza kwenda katika timu nyingine ya kawaida isiyo na presha. Angeweza kufunga walau mabao saba kwa msimu yangeitosha timu hiyo. Iwe Coastal Union au Namungo ama Tanzania Prisons. Angeweza kufanya hivyo.

John Bocco dhidi ya Yanga SC

Bocco angesimama mbele katika timu ambayo inamtegemea ambayo inaamini katika ustaa wake. Ambayo ina mashabiki wachache wanaomtegemea angeweza kurefusha urefu wa maisha yake ya soka mpaka kufikia miaka 40 kuliko kujidanganya kuwa kocha.” — Edo Kumwembe.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

CC: SportsArena, Wasafi media

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents