Habari

Epuka msongo wa mawazo unaohusiana na kazi

Maeneo mengine ya kazi, msongo wa mawazo ni kitu cha kawaida kulingana na aina za kazi. Msongo wa mawazo unaweza kuleta matatizo kama haujashughulikiwa ipasavyo. Namna unavyoshughulikia huo msongo ndivyo utakavyoleta mabadiliko. Watu wengi wanafikiri hawawezi kuongoza na kusimamia mazingira ya kazi zao, ndio huwezi kusimamia kila kitu kikaenda sawa, ila linapokuja suala la msongo wa mawazo unahitaji kuchukua hatua ya kukabiliana na hali husika hapo kazini.   

Kama una kazi nyingi unaweza kujikuta unatengeneza tabia usumbufu au kuwa mkali na kucharuka bila sababu. Unaweza kupoteza mwelekeo wa kazi yako pamoja na ujasiri uliokuwa nao hapo kabla, inakupasa kushughulikia msongo wa mawazo mapema ili uweze kupambana na hali ngumu.

1. Pangilia kazi zako vizuri

Hakikisha unajua majukumu yako ya kila siku kazini na ofisini, pangilia kipi kianze na kipi kinafuatia. Vile vile unapaswa kujua kila jambo litatumia muda gani na uweke mlinganyo sawa kati ya kazi na familia. Hakikisha unalala kati ya masaa 6 hadi 8 kila siku na kula vizuri.

2. Usifanye kazi masaa mengi zaidi

Sio rahisi kufanya kazi kwa masaa nane au tisa mfululizo. Watu wengi hufikiri wakiachwa kwa muda mrefu bila kuingiliwa na mambo mengine watamaliza kazi, hii si kweli ila uwezo wako wa utendaji utaanza kushuka. Hivyo basi pangilia vitu kulingana na umuhimu, kitu ambacho si cha lazima siku hiyo usikifanye fanya mambo ya muhimu na yanayohitajika kwa siku hiyo.

3. Fika ofisini mapema

Ukiwahi unaondoa hofu ya kuchelewa na kuwahi kwenye kiti chako, anza siku ukiwa na hali nzuri ya utulivu ni pamoja na kuwahi kufika. Hutaanza kazi kwa mawazo ya kwanini umeshelewa au bosi wako atakuonaje n.k  

4. Pangilia muda wako wa mapumziko ya kila siku

Unaweza kutoka na kutembea kwa dakika tano, ongea na wafanyakazi wenzako wakati wa mapumziko hayo ili kuiweka akili yako sawa na uweze kuendelea na kazi.Wakati wa chakula cha mchana usilie mezani kwako, nenda sehemu tofauti na dawati lako la kazi ambayo itakufanya kutizama vitu kutokea eneo jingine kimazingira. Kumpumzika kwa namna moja ama nyingine inakufanya kukuongezea nguvu ya kuendelea na kazi.

Kama tangazo la dawa “maumivu yakizidi mwone daktarri” Hivyo msongo wa mawazo ukikuzidi, usife na tai shingoni omba ushauri uweze kusaidiwa. Maisha yako yanathamani kubwa kuliko hicho unachokifanya ofisini kama hakina tija kwenye afya yako na maisha yako kwa ujumla.  

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents