Burudani

Exclusive: Fid Q kutoa ‘mini documentary’ ya ‘Siri ya Mchezo’ ambamo maprofesa watafanya uchambuzi

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amesema mashabiki wasitarajie kuona video ya wimbo wake mpya, ‘Siri ya Mchezo’ aliomshirikisha Juma Nature. Badala yake, atatoa mini documentary ya wimbo huo.

Mwana FA, Fid Q, AY, Arthur na mshikaji

“Hatutoi video ya Siri ya Mchezo, isipokuwa tunatoa mini documentary ambamo ndani tunatarajia kuwa na maprofesa, dakika 15, watachambua wao,”Fid aliiambia Bongo5.

Alisema kazi ya utengenezaji wa documentary hiyo itamalizika ndani ya wiki mbili zijazo.

Fid aliongeza kuwa ameamua kutoa mini documentary na si video ya Siri ya Mchezo ili watu waweze kuelewa zaidi dhana ya Kitaaolojia ambalo ni jina la albam yake ijayo. Msikilize hapo chini.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/117443479″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents