Burudani

Exclusive: Hemedy PHD ataja sababu 4 za kupenda kuvaa suti kwenye video zake

Hemedy PHD amelazimika kueleza sababu zinazomfanya apende kuvaa suti kwenye video zake nyingi.

web

Muimbaji huyo wa Imebaki Story ameiambia Bongo5 kuwa amelazimika kuzungumza kwakuwa mashabiki wengi wameendelea kumuuliza swali hilo.

“Kwanza ningependa watu watambue kila mtu ana style yake ya kuvaa na inayomvutia na kumpendeza,” anasema Hemedy.

2015
Picha ya mwaka 2015 ya Hemedy akiwa kwenye suti

“Pili ni kutokana na kuwa inspired na watu wanaovaa kigentleman kama Ne-Yo na Pitbul na Jidenna. Hawa hasa wamechangia sana mimi kupenda kuvaa muonekano huu ambao mtu yoyote anapenda na kuonekana presentable mbele ya watu,” ameongeza.

2013
Picha ya mwaka 2013 ya Hemedy akiwa kwenye suti

“Tatu ni style yenyewe ni timeless kutokana na kuwa hata uvae suit mwaka 1961 na uvae 2020 thamani yake haishuki na hazitoki nje ya fashion.”

2014
Picha ya mwaka 2014 ya Hemedy akiwa kwenye suti

“Nne ni bei yenyewe. Thamani ya suit ni kubwa so kwa mimi nimechagua kuvaa expensive coz I wanna look expensive,” amesisitiza Hemedy.
Jeans na t-shirt kwa bongo haizidi laki moja, ila suit moja inaenda kuanzia $450 hadi 1000.

Uvaaji wa t-shirt na jeans na style zingine unapelekea leo umevaa kesho mtu kavaa hata kikipitwa na fashion haivutii tena machoni, ila suit hata mvae watu 100 kwa pamoja hakuna atakaesema mmeigana. Ila mkifanana t-shirt sehemu watu wawili utatamani uvue ukimbie”

2012
Picha ya mwaka 2012 ya Hemedy akiwa kwenye suti

“It’s about classy and looking gentle, that’s my style.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents