Burudani

Flora Mbasha kuolewa na kuzindua albamu mpya siku moja.

Aliyekuwa Mke wa Muimbaji wa Muziki wa Injili Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha aka Madame Flora, anatarajia kufunga ndoa na mume wake mtarajiwa Daudi Kusekwa katika bustani za hoteli ya Rock Beach jijini Mwanza.

Madame Flora alisema kuwa ndoa hiyo itaambatana na uzinduzi wa albamu yake mpya inayoitwa ‘Wakati Wake’ pamoja na kitabu alichokipachika jina la ‘Siri za Flora Mbasha.’

“Ndoa itafungwa asubuhi na jioni kutakuwa na sherehe ya harusi, utambulisho wa albamu yangu mpya pamoja na kitabu kipya. Watu wote wanakaribishwa, ingawa kadi zimebaki chache tu kutokana na idadi ambayo imepangwa na kamati,” alisema Flora.

Chanzo Mtanzania.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents