Habari

Fukuto la Kuhama vyama likiendelea: Diwani mwingine Chadema akimbilia CCM leo

Fukuto la  madiwani wa Chadema kujivua uanachama na kujiunga na CCM limezidi kuongezeka baada ya leo Januari 27  Diwani wa Kimara (Chadema), Pachal Manota kukihama chama hicho na kuhamia CCM.

Manota amepokelewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba  wakati wa ufunguzi wa kampeni za jimbo la Kinondoni zilizofanyika viwanja wa Biafra, jijini Dar es salaam.

Diwani huyo ametambulishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na kukabidhiwa kadi papo hapo na kuomba kukubaliwa kuingia CCM huku akiomba radhi kwa wana CCM kumsamehe kama aliwahi kuwakosea.

Hata hivyo viongozi wa Chama Chama waliokuwepo walimkaribisha diwani huyo kwa furaha na kumkaribisha rasmi CCM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents