Habari

Fungeni mkanda muda wote muwapo safarini

Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe amewataka abiria wanaosafiri barabara ya Tunduma – Mbeya na wanaotoka nje ya Mkoa wa Songwe kufunga mkanda ili kuepuka madhara ambayo yanayoweza kuepukika.

Kauli hiyo ameitolewa Mei 07, 2024 wakati akifanya ukaguzi wa magari eneo la Chimbuya wilayani Mbozi na kueleza umuhimu wa kufunga mkanda pindi abiria awapo safarini ili kujihakikishia usalama wake.

“Mnatakiwa kufunga mkanda ili endapo inatokea ajali uwe salama lakini usipofunga mkanda utashindwa kujizuia na itakutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine na kusababisha madhara kwa watu wengine kwa hiyo abiria nawaomba fungeni mkanda wakati wote unapokuwa safarini toka unapoingia kwenye gari funga mkanda, ukitoka kula na kuchimba dawa funga mkanda ili uwe salama wewe na mwingine” alisema SSP Bukombe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents