Burudani

G-Nako adai ubinafsi ni chanzo cha makundi mengine kuvunjika

Rapper wa kundi la Weusi, George Mdemu maarufu kama G-Nako, amesema umoja, upendo pamoja na nidhamu kunalifanya kundi hilo kuendelea kustawi.

IMG_0726 (800x533)

Rapper huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa kufanya kazi kwa kushirikiana kunalifanya kundi hilo kuendelea kufanya vizuri.

“Sababu hizo tuliziweka kwa pamoja wakati tulipoanzisha kundi letu hilo ambalo kwa sasa ni kampuni. Makundi mengi yanasahau kwamba nidhamu ni kitu muhimu katika kila kazi, wengi wao hujitazama binafsi husahau mafanikio ya kundi, huja kwa kuzingatia misingi hiyo tunayotumia sisi na kujikana mwenyewe kwamba ni zaidi ya wenzako,” alisema Nako.

“Pia sisi tuna kitu kimoja tunakiita heshima kwa mdogo na mkubwa ndiyo maana hatukatai ushari wa yeyote hata ukiwa wa kutuponda tunafanyia kazi ili tukitoka awamu nyingine yule aliyetuponda awe mshabiki wetu, hatupunguzi mashabiki bali tunaongeza.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents