Ganang Style ya PSY yafikisha views bilioni 1 kwenye YouTube
Video ya wimbo wa PSY, “Gangnam Style” imekuwa video ya kwanza katika historia ya internet kuangaliwa kwa zaidi ya mara bilioni moja kwenye mtandao wa YouTube.
Tangu ifikishe rekodi ya views milioni 803 kwenye YouTube, “Gangnam Style” imekuwa ikiangaliwa kwa mara milioni 6.5 kwa siku ama views 76.4 kwa kila sekunde.
Ukilinganisha na video ya pili iliyoagaliwa zaidi ya Justin Bieber , Baby haiwezi kufikisha views bilioni 1 hadi mwaka 2014, kwa mujibu wa makadirio yaliyofanywa na Next Big Sound.
Yenyewe imekuwa ikiangaliwa mara 300,000 kwa siku sawa na views 3 kwa sekunde.