Habari

Halima Mdee kuiongoza tena BAWACHA baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti kwa muda huu

Halima Mdee kuiongoza tena BAWACHA baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti kwa muda huu

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), baada ya kupigiwa Kura za Ndio 317 kati ya Kura 324.

Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

Matokeo ya Uchaguzi huo yametangazwa leo Disemba 13, 2019, ambapo kupitia ukurasa wa Twitter wa chama hicho ukatoa mchanganuo wa Mwenyekiti pamoja na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ulioanza jana asubuhi, umemalizika asubuhi hii ambapo umemchagua Halima Mdee kuwa Mwenyekiti wa Bawacha Taifa” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha katika Uchaguzi huo Hawa Mwaifunga, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bawacha Tanzania Bara, huku Sharifa Suleiman, akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents