Burudani

Harmonize afunguka haya kuhusu mapromota wa Kenya baada ya sakata la kushindwa kutumbuiza moja ya show zake chini Kenya

Harmonize afunguka haya kuhusu mapromota wa Kenya baada ya sakata la kushindwa kutumbuiza moja ya show zake chini Kenya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmonize ‘Konde boy’ jinsi anavyojiita kwa sasa,amefunguka mwanzo mwisho na kutoa hisia zake kuhusu mapromota kutoka nchini Kenya.

Harmonize ameongea hayo leo akifanya mahojiano na BBC Swahili katika jiji la Nairobi nchini Kenya huku akiahidi mwisho wa mwezi huu ataachia moja ya wimbo anaoukubali sana.

Baada ya kuulizwa vipi kuhusu kufanya show tena Kenya baada ya lili sakata la kuzulumiwa malipo na moja ya promota ambaye alikimbia na pesa zako na wewe kushindwa kufanya show;-

Harmonize alijibu hivi;- ” Mimi ntafanya kazi kama mapromota watakuwa tayari kwa ajili ya kazi na kama watanihitaji maana moja ya nchi ambazo nini mashabiki wengi mno ni Kenya, Kwahiyo siwezi kuacha kufanya show hapa Kenya ila inategemeana na mapromota watakavyojipanga ntafanya sho”

Huku akiongezea :- ” Mbali na hilo mwezi decemba nina show yangu ntaifanya Mombasa kwa maana hiyo bado naendelea kufanya kazi na watu wa Kenya”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents