Michezo

Hii ni aibu kwa Simba – Edo Kumwembe

“Sasa msimu umemalizika dhahiri kwa Simba. Sioni namna gani Simba wakichukua ubingwa kwa pengo la pointi lililopo. Baada ya Azam kucheza dakika 90 na za nyongeza dhidi ya Mashujaa bila ya kufunga bao lolote Ijumaa usiku sioni namna gani Yanga wanaweza kuzuiwa wasitwae ubingwa.

Swali ni namna gani Simba watarudi msimu ujao. Wamejifunza kitu au wataendelea kumdharau Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said? Watafumua kikosi chao cha utawala wa timu? Watarekebisha mipango yao ya usajili wa timu na kuleta wachezaji wenye hadhi ya Simba katika kikosi? Ni suala la kusubiri kwa sasa. .

Tupo Aprili. Mvua zinanyesha. Tusubiri Aprili ya mwakani kuona Simba itakuwa wapi. Kuona itakuwa imejirekebisha wapi. Leo ni aibu kuona baadhi ya mashabiki wa Simba wakiwa wanapumua baada ya kufungwa na Yanga. Kisa? Eti wamefungwa mabao machache kuliko walivyotazamia. Aibu.” — Edo Kumwembe.

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents