Burudani

Hiki ndicho Nahreel atakachokuwa akikifanya kwenye Coke Studio mwaka huu

Producer wa The Industry na member wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel anajiunga na kipindi cha Coke Studio Afrika kama producer katika msimu mpya ulioanza jijini Nairobi, Kenya.

20150528045211

Kazi ya Nahreel ni kutayarisha nyimbo zitakazoimbwa na wasanii wa msimu huu wa tatu.

“Nimepewa kazi kubwa kidogo, nilishaanza kuiandaa tokea miezi miwili iliyopita,” Nahreel ameimbia Bongo5.

“Ni utengenezaji wa mash ups, mash up ni ku-combine nyimbo mbili kuwa one song without kupoteza ladha. Mimi natengeneza halafu na submit to the band under my supervision and band wanapiga the way I made them.”

Producer huyo amesema ni kazi zake za mwaka jana ndizo zimemfanya achaguliwe kuungana na jopo la watayarishaji wa show hiyo.

“Nadhani walifuatilia kazi yangu, wakaona ninafaa kwa hiyo kazi. Vanessa na Joh Makini ni wasanii ambao nimeproduce kazi zao na mwaka jana walishiriki vizuri kwenye coke studio nahisi pia iyo ilichangia.”

Ben Pol, Alikiba na Vanessa Mdee ni wasanii kutoka Tanzania watakaoshiriki kwenye msimu huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents