Habari

Hisa moja ya Twitter yauzwa kwa zaidi ya shilingi 73,000

Hisa za mtandao wa Twitter jana zimeuzwa kwa $44.90 (zaidi ya shilingi 73,000) ikiwa ni asilimia 73% zaidi kutoka kwenye bei yake ya kwanza ya $26 kila moja.

twitter-stock-twtr-execs
Waasisi wa Twitter Jack Dorsey, Evan Williams na Biz Stone wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya hisa za Twitter kuingia (IPO) jana

Hiyo ina maana kuwa baada ya siku ya kwanza ya kampuni hiyo kuwa ya umma, Twitter sasa inathamanishwa kwa dola bilioni 31.

Zaidi ya hisa milioni 13 ziliuzwa saa moja tu baada ya kuingia sokoni kufutia soko la hisa la New York kufunguliwa.

Twitter ina watumiaji milioni 230 lakini bado haijaanza kupata faida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents