Habari

Hizi ni tabia za mabosi zinazowafanya watu kuchukia kazi

Tabia ni moja ya vitu ambavyo mtu huwa navyo na mara nyingi huonekana vizuri maeneo ya kazi, ila huwa hatujui zinaharibu vipi utendaji wa kazi. Tabia za mabosi wao zinapokuwa si nzuri hawawezi kusema kokote kwa kuhofia kufukuzwa kazi, hivyo wafanyakazi wazuri kwenye kampuni nyingi hutafuta kutoka kwenye hiyo kampuni. Kwakuwa mabosi wengi wanachoangalia ni uzalishaji, bila kujali utazalisha kwa nguvu gani, unahitaji nini na masaada gani bali hutaka matokeo makubwa zaidi, kuwaacha wafanyakazi kwenye hatihati.

boss

Kama wewe ni bosi wa kitengo fulani na watu wengi wamekuwa wakiaacha kazi, ni wakati wa kufikiria tabia yako na unaongoza vipi walio chini yako. Vile vile kazi yako itakuwa matatani kwani kazi hazitaenda vizuri, jiulize kwanini watu wananikimbia? Watu hawakimbii kampuni kwa sababu kampuni ni mbaya ila ni kwa sababu ya mabosi ni mabaya.

Inawezekana kuna tabia kama hizi kwenye kitengo chako;

1. Wewe huwafanya watu wafanye kazi masaa mabaya.
Je watu wa kitengo chako wanafanya kazi mpaka saa ngapi? au wewe huwa unawapa majukumu muda gani? Je ni asubuhi au wakati wa mchana? Au jioni muda mchache kabla ya muda wa kazi kuisha na unataka hiyo kazi ifanyike na uipate siku hiyo hiyo?

2.Je unawatoa wafanyakazi wako kafara?
Simaanishi kuwaua, bali namaanisha jambo au tatizo likitokea unalitatua vipi? au unawasukumia wafanyakazi wako ili na wewe mabosi wako wasijue kama huwa unakosea? Huko ni kukwepa majukumu yako unapofanya kosa.

3. We siku zote huona watu hawajafanya vizuri
Ni vizuri uwashauri waliochini yako namna ya kufanya vizuri kuliko kuwafokea au kupayuka unapoongea nao. Kupayuka kwako wewe kunaonyesha jinsi gani unavyotaka kazi ifanyike vizuri bali kwa wafanyakazi ni kuwakosea heshima.

4. Huwapi fursa ya kukua kitaaluma
Kazi zote zinaboa endapo tu hakuna kukua ndani yake au kupelekwa viwango vingine. Wafanyakazi wako wanapokuwa wameboreka ndipo matatizo huanza. Je unampango gani wa kukuza taaluma zao?

5. Huwalipi vizuri
Wafanyakazi wengi hawafurahii kazi zao kwasababu kinachoonekana kutokulipwa vizuri au kutotendewa haki katika malipo. Na jambo hili linachangia kwa kiasi kikubwa watu kuacha kazi au kubadilisha kazi.

Je wewe unafikiri nini kuhusu nafasi uliyonayo kwenye kitengo chako? Je watu wanapenda kufanya kazi na wewe? Je watu wanakaa kwenye kitengo chako au wanakimbia? Je wajua kwanini  wamekimbia?

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents