Habari

Homeboyz wamshataki promoter ‘fake’ wa Keri Hilson


Kampuni ya burudani ya nchini Kenya ya Homeboyz inamshtaki mfanyabishabiasra mmoja wa Kenya kwa kuwatapeli mamilioni ya shilingi kwa kudai kuwa angewapeleka wanamuziki wa Marekani Usher na Keri Hilson kwenye tamasha la Tusker All Star jijini Nairobi, October 1, mwaka jana.
Homeboyz walimlipa mfanyabiashara huyo Thomas Joseph Okeyo shilingi milioni 14.2 za Kenya ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 250 za Tanzania ambaye aliwalaghai kuwa angewapeleka wasanii hao wa kimataifa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Okeyo, anadaiwa kuwa alichukua fedha hizo kwa ulaghai na kudai kuwa angeweza kuwapata wasanii hao kwaajili ya show ya kampuni ya East African Breweries lakini Keri Hilson alikanusha kupitia Twitter kuwa hakuwa booked kwa show hiyo.
Baada ya kesi hiyo kwenda mahakamani ilikuja kubainika kuwa nyaraka zilizotumika kama mkataba wa makubaliano hayo zilikuwa fake na hivyo mtuhumiwa kushikiliwa na polisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents