BurudaniDiamond Platnumz

Huu ndio mpango wa ex wa Zari na mpambe wake wa kutaka kuharibu furaha ya ujio wa Tiffah

Ulimwengu una maajabu mengi na mitandao ya kijamii inatusaidia kuyafahamu. Uhusiano wa Diamond na Zari the Bosslady haujawahi kupokelewa vizuri na ex wake Ivan aliyezaa naye watoto watatu wa kiume.

11375421_860981820656919_922632704_n
Ivan (kulia) akiwa na mpambe wake King Lawrenc (kushoto) na Jose Chameleone

Watoto hao wameendelea kuwa karibu na wazazi wote wawili.
Uhusiano wa ulipoanza tu, Ivan kupitia mpambe na rafiki yake wa karibu, King Lawrenc walianzisha vita kwenye mitandao ya kijamii kuwashambulia Diamond na Zari. Hakuna shaka kuwa Ivan amekuwa akionesha hisia zake za kutoupenda uhusiano wao kupitia Lawrenc ambaye amekuwa akiwashambulia mfululizo.

Katika kipindi ambacho tension kati ya Diamond na Alikiba zimefika kileleni hususan kipindi cha kuelekea tuzo za KTMA 2015, Ivan mwenyewe pia alishiriki katika kampeni za kumuombea kura Alikiba. Ni wazi kuwa Ivan bado hajakubali yaishe, na kumuona mke wake wa zamani akiwa na furaha na Diamond ni kitu kinachomkera zaidi.

Na sasa wakati uhusiano wa Diamond na Zari upo katika kilele cha furaha baada ya kujaaliwa mtoto wa kike, Latiffah, kambi ya Ivan kupitia mpambe wake Lawrenc imedhamiria kuitilia doa furaha hiyo.

King Lawrenc ameanza kutupa mashambulizi kwa Diamond na kueleza kile anachoamini kuwa Tiffah ni mtoto wa Ivan! Kwa historia ya kile Lawrenc amekuwa akikisema tangu mastaa hao waanzishe uhusiano, ni wachache wanaoweza kuamini ‘upuuzi’ huu lakini kiukweli hiki ni kitu kinachoweza kuwakosesha raha Diamond na Zari, kama wakiamua kumjali.

Lawrenc alianza kupost picha ya mtoto mchanga na picha ya Ivan na kuandika, “No DNA Needed. The best revenge has shown itself after 9months. Anamaanisha kuwa mtoto huyo ni Tiffah na kwamba Ivan ndio baba yake.

Hadi sasa hakuna picha iliyotolewa inayoonesha sura halisi ya Tiffah hivyo ni ujinga kuamini kuwa aliyoweka Lawrenc ni yake. Na katika yote yanayoondolea, Zari na Diamond hawawezi kuruhusu picha ya mtoto wao ifike kwenye mikono ya adui yao labda kama wao wenyewe wakiamua kuipost kwenye mitandao ya kijamii, kitu ambacho bado hawajakifanya hadi sasa.

Na pengine mambo kama haya ndio yanamfanya mama mzazi asite kuionesha sura ya binti yake huyo. “I swear I wanted to show you her face but she turned away saying, nope i want no drama. She knows y’all can be dramatic. She’d rather stay safe for now… too many judges, advisors, teachers you name it you’ll find it on IG. I bet she can’t deal,” aliandika Zari.

11849036_814421318655954_302602293_n

Lawrenc hakuishia hapo, siku tano zilizopita, alipost picha Instagram akiwa na Ivan na kuandika, “Chilling with @princess_tiffah’s father.” Caption hiyo ilizua hasira kubwa kutoka kwa mashabiki na wengi wamemshangaa Ivan kwa kumruhusu mpambe wake kueneza maneno ya kipuuzi katika suala nyeti kama hilo.

20150814012704

Lakini ni comment moja ya shabiki mwenye hasira inayoweza kuwafanya Ivan na Lawrenc kufikiria tena mpango wao huo.

“@ivandon, you know, I thought you were one cool guy, but you are a pimp how could you hang out with gays? are you by any chance @kinglawrenc ‘s boyfriend? / girlfriend ? So you did not move on yet huh and it hurts you so much to see zari with a man and not a sucker like you was to her huh? it hurts you that the man she is f*ckinh now is a man enough to make her gve birth to a baby girl do you know why she did nat had a girl bfo? because you were coming so fast during sex you can’t f*ck for ten seconds , now she has a man that can make her come ten times in ten seconds thats why you see a baby girl as an outcome and it kills you that you couldn’t f*ck her enough, f*ck you.”

Hakuna shaka kuwa Ivan na Lawrenc wataendelea kuhakikisha kuwa wanamtumia Tiffah kama silaha ya kuwaumiza Zari na Diamond japo kwa upande mwingine hatuoni kama wawili hao wanajali. Picha zinaonesha wazi kuwa Tiffah ameleta furaha kubwa kwenye familia ya Chibu.

11356964_411869189006246_794661119_n

“Asante Mwenyez Mungu kwa kuendelea kunilindia Upendo, Amani na Furaha ya Familia yangu,” ameandika Diamond kwenye picha inayomuonesha akiwa jikoni na mchumba wake na mama yake aliyembeba malaika wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents