Burudani

Idris kumfanya Goitse shemeji/wifi yetu? Wala dinner ya wawili

Siku washiriki wa BBA Hotshots wanatambulishwa, mwakilishi wa Tanzania, Idris Sultan alimwambia mtangazaji IK kuwa cheche zake zipo kwenye masuala ya wanawake. Huenda sasa shughuli imeanza.

10702146_833956386625236_6706908967660485281_n

Idris aliamua kuwa na dinner ya pamoja na mwakilishi wa Botswana, Goitse, thanks kwa housemates waliompa nafasi hiyo. Nhlanhla na JJ walisaidia kupika chakula kuhakikisha kuwa wawili hao wanakuwa na mtoko aka date utakaowafurahisha.

Wakati wote wa dinner, Ellah, Sabina, M’am Bea na Luis walishiriki sehemu yao ya kuwahudumia chakula. Idris alimuuliza Goitse maswali kutaka kumfahamu zaidi na kumuuliza kama anaamini katika uhusiano wa mbali, long-distance relationships.

Idris alikuwa anaelekea kuzalisha uhusiano wa kimapenzi ndani ya nyumba? Goitse, hata hivyo alionesha kuvutiwa zaidi na urafiki zaidi.

Mhh! Tunaweza kupata shemeji/wifi mwingine kutoka Botswana baada ya O’Neal na Feza Kessy mwaka jana? Hilo litawezekana kama tutamuokoa Idris kwenye hatari ya kutoka wiki hii. Tuma neno Idris kwenda 15426.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents