Burudani

Inspekta Haroun kuja na ngoma mpya, ‘Mong’onyomong’onyo

Rapper wa TMK, Kahena Haruna aka Inspekta Haroun amesema ngoma yake ijayo itaitwa ‘Mong’onyomong’onyo’ yenye maana ya muhogo mtamu uliofananishwa na binti za kizaramo mwenye tabia njema.

INSPECTOR.INSPECTOR.

Inspekta ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo umeimbwa katika lugha ya kizaramo ambayo ni lugha ya mama yake.

“Lugha la mama yangu, yaani nimezungumzia kuna muhogo mmoja unaitwa kibanga meno au ‘Mong’onyomong’onyo’ ni muhogo mzuri sana huu, sasa ule muhogo ukiuchemsha unaiva vizuri hata ukiupika na nazi yani ni muhogo ambao unapendwa sana. Kwahiyo nimezungumzia binti kwa tafsiri ya huo muhogo yaani binti uzuri wake ni sawa na huo muhogo hauchoshi kula, hata ukila leo utatamani kila siku kama unavyokula wali hauchoshi,” amesema rapper huyo.

“Kwahiyo nimezungumzia binti ambaye ana tabia njema, ambaye amelelewa na wazazi, ameishi vizuri, lakini huyo binti hataki kuchezewa, yeye anachotaka ni posa, kwahiyo uzuri wake ni ‘Mong’onyomong’onyo’ ndo maana wimbo ukaitwa hivyo. Wimbo upo tayari na utatoka siku yoyote ila masuala ya production na nini nitazungumzia siku ya kutoka.

Kwa upande mwingine Inspekta ameeleza kwanini hupenda kuzungumzia vyakula kwenye ngoma zake.

“Masuala ya chakula kwenye nyimbo zangu ni kama identity yangu. Wengine wanapenda kutaja pombe lakini mimi ni masuala ya vyakula, lakini kwa sababu mwili haujengwi na matofali na kuna siku ya chakula duniani, kwahiyo mimi nimeona kwenye nyimbo zangu sio mbaya kuzungumzia masuala ya msosi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents