Burudani

Jafarrai awataka madj kuweka usawa kati ya nyimbo za rap na zile za kuimba

Rapper, Jaffarai amedai kuwa muziki wa Tanzania umekuwa na changamoto ya nyimbo nyingi kutopata rotation ya kutosha huku akidai hali hiyo inasababishwa na madj kushindwa kuweka uwiano kati ya nyimbo za kuimba na zile za rap kwenye playlist zao.

10914226_798395506864533_386696199_n

Akizungumza na Bongo5 leo, Jaffarai amesema sasa hivi wasanii wanafanya muziki mzuri kilichobaki ni kuzipa rotation kazi zao na kuacha kushabikia kazi za nje.

“Wadau wote wanatakiwa kuongeza rotation ya upigaji wa nyimbo nyingi za Bongo,” amesema rapper huyo.

“Muda mwingi Djs na radio mbalimbali wanapiga nyimbo nyingi za kuimba na kuacha za kurap. Rap zinapigwa kwenye vipindi vichache sana. Nyimbo nyingi za kuimba ndo zinapigwa muda mwingi sana yaani zinapata rotation kubwa sana kuliko za kuimba. Kwahiyo wanatakiwa kuongeza rotation kila kipindi kiangalie uwiano mzuri wa nyimbo pia wajaribu kupunguza kupiga nyumba za nje sana na sasa waanze kupiga nyimbo za ndani hiyo nitakuwa ni njia sahihi ya kuokoa muziki wa rap,” ameongeza Jaffarhymes.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents