Habari

Jaji Upendo afariki dunia

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye alijiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia,” amesema Mbaga.

Aidha amesema marehemu ameacha watoto wanne.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents