Michezo

Adnan Januzaj kurudi Manchester United

Klabu ya Manchester United imemrudisha nyumbani mchezaji wao Adnan Januzaj kutoka Borussia Dortmund ambako amekuwa kwa mkopo wa msimu mmoja.

2F406C5300000578-0-image-a-20_1449849612282

United wamemtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji arejee Old Trafford kwa sababu ya kukosa nafasi ya kuchezeshwa huko Ujerumani.

Januzaj, mwenye umri wa miaka 20, hadi sasa amecheza mechi 12 pekee katika klabu hiyo ya Bundesliga, sana akiingia kutoka benchi kama nguvu mpya.

Ni mara tatu pekee ndo alikuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi.

Mechi zote alizochezeshwa katika ligi, ambazo ni mechi sita, aliingia kama nguvu mpya.

Hajachezeshwa hata mara moja tangu mechi ya Europa League ambayo walichapwa na PAOK Salonika tarehe 10 Desemba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents