Habari

JATU yaitisha mkutano wa zoom wa dharura, wanahisa waombwa kushiriki

KAMPUNI ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini (JATU) PLC imeitisha mkutano maalum na wadharura kwa lengo la kuwakutanisha wanahisa zaidi ya 10,000 wa kampuni hio ili waweze kuwapitisha wajumbe wa bodi ambao hatua za kuwapata zilishafanyika kisheria.

Mkutano huo wa dharura wa JATU utafanyika kwa njia ya mtandao (zoom) kesho na unakuja wakati ambao kampuni hiyo inapitia changamoto mbalimbvali ikiwemo ukosefu wa fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu JATU Plc, Mohamed Simbano anasema watu watakaoudhuria kwenye mkutano huo ni wale wote wenye hisa katika kampuni hiyo.

Anasema kwa wanahisa ambao watashindwa kuhudhuria au kuteua mwakilishi watapaswa kutuma fomu za uwakilishi mapema kabla ya siku ya kesho.

“Watakaoshiriki mkutano huu ambao utafanyika kwa njia ya mtandao hapo kesho ni wale wanahisa tu, tunataka wanahisa washiriki kuwapitisha wajumbe wa bodi ili kuruhusu wafanye kazi ya kuweza kuirudisha kampuni yetu kwenye uzalishaji,” anasema Simbano

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu JATU Plc, Mohamed Simbano

Anasema wanafanya mkutano huo mara baada ya kumleta mtaalamu wa masuala ya biashara, fedha na utawala kutoka Uholanzi, Ben Philpsen aliyekuja kwa njia ya kujitolea ili kuisaidia kampuni hiyo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo madeni.

“Kila mwanahisa wakati wa kuingia katika mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya mtandao yaani zoom lazima aandike jina lake sahihi kama linavyosomeka kwenye cheti chake hisa ili uongozi uweze kupitia na kuthibitisha kama kweli ni mwanahisa kinyume na hapo ataondolewa kwenye kikao.

“Nia yetu ni njema tunataka kila mtu aweze kushiriki kwakuwa hatutaki mwanahisa yeyote apoteze haki yake ya msingi ya kupiga kura kuchagua wajumbe pindi itakapofika,” anasema Simbano

Anasema mara baada ya mkutano huo kufanyika na kupata wajumbe wa bodi watakuwa na jukumu la kurudisha kampuni kwenye uzalishaji na ndani ya miezi mitatu wataitisha mkutano mkuu ambao utafanyika katika ukumbi mkubwa hivyo wanahisa wote watahudhuria na kutoa maoni yao.

“Baada ya mkutano wa kesho sasa bodi pamoja na viongozi watakuwa na jukumu la kurudisha JATU kwenye uzalishaji na ndani ya miezi mitatu wataitisha mkutano mkuu ambao utafanyika kwenye ukumbi mkubwa maana tutakuwa na uwezo wa kumudu gharama ndogo ndogo za kila siku katika endeshaji ambazo kwa sasa zimesimama.

“Mkutano huo mkuu kila mwanahisa atahudhuria na utakiuwa na ajenda zisizopungua 15 ikiwemo mwenendo wa kampuni, hatma ya madeni, magawio ya hisa, miradi na mambo mengine ya utendaji wa kampuni kwa ujumla,” anasema

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents