Jay z na Beyonce wanunua gari ghali zaidi duniani ‘Rolls-Royce Boat tail’ (+ Video)

Msanii tajiri zaidi kwa sasa duniani Jay Z ambaye anakadiriwa kuwa na utaji wa 1.4 billion USD sawa na takribani Tsh trilioni 3.2466 pamoja na mpenzi wake Beyonce Hivi karibuni ilielezwa kuwa wameiomba kampuni ya kutengeneza magari maarufu na ghali duniani ya “Rolls-Royce” iliwatengenezee gari ambalo walilitambulisha kuwa ni aina mpya “Rolls-Royce Boat tail” ambapo walitaka litengenezwa wanavyotaka wao.

Taarifa za leo zinaeleza kuwa tayari Jay Z na bebi mama wake Beyonce wameshalivuta ndinga hilo nyumbani kwao ambapo gari hilo linaelezwa kuwa na thamani ya  dola za kimarekani milioni 28 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 65 ambapo imeelezwa gari hilo hadi kukamilika liligharimu zaidi ya miaka mitatu hadi kukamilika kwake.

Gari hili aina ya “Rolls-Royce Boat tail” walilolinunua Jay Z na Beyonce likitajwa kama ndio gari lenye Thamni zaidi duniani.

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/tv/CPiBmjyBNk6/

 

Related Articles

Back to top button