Burudani

Jay-Z na Rihanna kutumbuiza kwenye sherehe za ufungaji wa Paralympics


Jay-Z , Rihanna na kundi la Coldplay watatumbuiza kwenye sherehe za kufunga mashindano ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu Jumapili ijayo (09.09.12) jijini London Uingereza.

Gazeti la Daily Mirror limesema kuwa kiongozi wa Coldplay Chris Martin ndiye aliyemshawishi Jay-Z kushiriki.

Vyanzo vimesema show hiyo inategemea kuhudhuriwa na mashabiki wengi wa wanamuziki hao na kwamba sherehe hizo za ufungaji wa Paralympics zitafana kuliko miaka ya nyuma.

Mashindano ya Paralympics huanza muda mfupi baada ya kumalizika kwa Olimpiki ya kawaida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents