Burudani

JB adai anajali heshima kuliko pesa kwenye filamu

Muigizaji wa ‘Chungu cha Tatu’ Jacob ‘JB’ Stephen amesema yupo tayari kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 200 kwenye filamu bila kujali hasara ili kujenga heshima yake katika tasnia ya filamu.

JB

JB amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa, ameamua kuwaridhisha mashabiki wake wa filamu kwa kufanya kazi za gharama za juu na zenye ubora.

“Mimi nimetengeneza sinema zaidi ya 37 mpaka sasa hivi kupitia kampuni yangu ya Jerusalem na pesa zipo kwenye akaunti yangu lakini kumbukumbu yangu kubwa ni filamu zile ambazo watu wameangalia. Kwahiyo kule kuuzungumzia uhusika wangu kwenye kazi zangu ndiyo kunanipa kichaa,” alisema.

“Nitafanya filamu kwa gharama yoyote hata iwe milioni 100 au 200 kwa hizi local movie nipo tayari hata kama haitarudisha ilimradi filamu iwe nzuri,” alisisitiza.

Pia JB amesema tayari ameshafikia makubaliano na moja ya TV kubwa kwa ajili ya kuonesha tamthilia yake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents