Burudani

Je unaijua historia ya Alikiba?? (video)

Mwamba huyu hapa ALLY SALEH KIBA alimaarufu kama @officialalikiba kutoka Kariakoo jijini Dar Es Salaam.

Jina lake alilopewa na Mashabiki kama Mfalme wa Bongo Fleva hawakukosea kabisa, muziki wake umekuwa chachu kwa vijana wengi kuingia kwenye muziki.

Amekuwa role model wa vijana wengi ingawa hawawezi kusema ila amewafanya wengi waingia kwenye muziki.

Mafanikio yake ya ndani na nje ya muziki kwa Takribani miaka 20 ndio yanamfanya Alikiba kuwa miongoni mwa wasanii bora wa muda wote Afrika Mashariki.

Muziki wake, sauti yake na uandishi wa mashairi yake yasiyoisha ladha ndio yanamfanya aendelee kulitawala game la Bongo Fleva mpaka sasa.

Alikiba ndio msanii pekee kutoka Tanzania aliyeaminiwa na R KELLY kuingia kwenye Project ya One8 iliyotoa ngoma ya HANDS ACROSS THE WORLD miaka 13 iliyopita ambyo ilihusisha wasanii mbalimbali wakubwa barani Afrika akiwemo 2Face Nigeria, Fally Ipupa Congo DR, Amani Kenya, Navio Uganda na wengine wengi.

Amefanya muziki kwa takribani miaka 20 bila kushuka na mpaka sasa anaendelea kukisumbua kizazi kipya.

Mpaka sasa ana Album tatu tu ambazo ni CIDERELLA, ALLY K FOR REAL & THE ONY ONE KING na anatajwa kama miongoni mwa wasanii waliofanikiwa kuuza kanda (copy) nyingi zaidi kupitia album ya CINDERELLA.

Mwaka 2016 alifanikiwa kushinda tuzo ya MTV EMA mbele ya Wizkid, Platnumz, Davido na wengine na pia ana tuzo mbalimbali za ndani na nje ya Nchi.

Juzi amezindua Radio yake ya Crown Fm lakini pia anamiliki lebo ya muziki na baadhi ya mambo mengine mengi.

Hayo ni baadhi tu kuhusu Alikiba na wimbo uliomfungulia dunia ni CINDERELLA na baada ya hapo THE REST IS HISTORY.

Hizo ni baadhi ya nyimbo zake alizowahi kufanya zamani na tuambie Wimbo gani unaupenda kutoka kwa Alikiba?? #HESHIMAKWALEGEND

Imeandaliwa na @el_mando_tz

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents