Burudani
Alikiba, Harmonize & Rayvanny kwenye orodha ya wasanii wanaolipwa zaidi

Jarida maarufu barani Afrika la African Fact Zone limetoa orodha ya wasanii anaolipwa kitita kirefu zaidi barani Afrika kwenye Show yako moja tu.
Katika Jaridas hilo limemtaja wakali kutoka Nigeria ambao Burna Boy, Wizkid, Rema kama vinara wa kulipwa mkwanja mrefu zaidi, wakali hao wanapokea dola milioni moja amazo ni zaidi ya Tsh bilioni 2.5.
Katika orodha hiyo pia imewataja wakali kutoka Tanzania kama vinara wanaoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki, Platnumz analipwa dola laki moja ambayo ni sawa na Tsh Milioni 250 huku Alikiba akifuata kwenye orodha akilipwa dola Efu Hamsini ambayo ni zaidi ya Tsh Milioni mia moja.
Harmonize anafuatia akilipwa dola Efu Ishirini na tano ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 50 huku Rayvanny akilipwa dola Elfu 20 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 40.
Swipe kuiona orodha hii