Michezo

Jobe na Fredy waachiwa mzigo Simba Kufuzu

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC  Abdelhak Benchikha amesema jukumu la kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika  liko chini ya Safu yake ya ushambuliaji.

Simba SC itakuwa wageni wa Al Ahly kwenye mchezo wa Mkondo wa pili wa robo fainali utakaochezwa Uwanja wa Cairo International nchini Misri kesho Ijumaa (April 5) ambao wekundu wa Msimbazi watahitaji ushindi wa zaidi ya bao moja kuingia nusu fainali.

Benchikha amesema ameikabidhi safu ya ushambuliaji jukumu la kuwapeleka nusu fainali kwa kutumia vizuri kila nafasi itakayopatikana kwenye mchezo wa kesho Ijumaa (April 5).

Kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita (Machi 29) ambao Simba SC walifungwa bao 1-0 washambuliaji wa timu hiyo walipoteza nafasi za wazi za kufunga kitu ambacho kimesababisha kocha huyo kuwasisitiza juu ya jukumu hilo.

Benchikha amesema alitumia siku 5 kuwapa mbinu na kuikumbusha safu ya ushambuliaji umakini wa kutumia nafasi zitakazopatikana katika mchezo huo, aliouita kuwa ni wa fainali kwao, kwani unabeba hatima yao ya kuingia hatua inayofuata.

“Tunahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kupata matokeo ya mechi kubwa, nina imani kile nilichowapa katika uwanja wa mazoezi ndani ya siku tano tunaweza kufanya vizuri ugenini” alisema Benchikha.

“Al Ahly ni timu kubwa hilo linajulikana wazi na ina wachezaji wenye uwezo mkubwa, nasi tunahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa katika kuendelea ushindani. Tumefanya kazi makosa tuliyofanya kwenye mchezo uliopita na ni matumaini yangu hayatajirudia kwenye mchezo huu” alisema Benchikha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdalah (Try Again) amesema wao ni wawindaji na wameenda kushindana na kutafuta ushindi ugenini dhidi ya wenyeji wao Al Ahly.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents