Burudani

Juma Nature: Kwenda international ndio nini?

Juma Nature amesema hana haraka ya kwenda kimataifa kwa kudai bado ana muda wa kutosha kwenda huko.

juma_nature

Nature anadai kuwa bado anajichukulia kama msanii mchanga mwenye kipaji cha ajabu.

“Hizo ni plan zangu baadaye sio sasa hivi,” Nature ameiambia Bongo5.

“Mimi sifanyagi kitu kwa kuiga, kwa sababu mimi sio underground na nina jina la kutosha lakini unaweza kunifananisha na underground mwenye kipaji. Nikiona watu wanashindwa kufanya vizuri nakaza ili niwaonyeshe Nature ni nani! Kwa sababu mimi kimataifa nilishafika huko wakati wa nyuma, kwahiyo mimi sio mshamba wa maisha hapa duniani. Vingi nimefanya kupitia sanaa kwahiyo hivyo wanavyofanya wenzangu naona ni mambo ya kawaida tu,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents