Burudani

Juma Nature: Uhusiano wangu na P-Funk utaendelea kuwa bora zaidi, hatujagombana (Video)

Sir Juma Nature amedai kuwa uhusiano wake na producer wa Bongo Records, P-Funk Majani ni mzuri na utaendelea kuwa bora.

Akiongea na Bongo5 njia wakati wakielekea Musoma kwenye Serengeti Fiesta, Nature amesema amepunguza kurekodi kwa Majani kwakuwa ana studio yake lakini bado wana uhusiano mzuri.

“Sijatokea muda mrefu sana kufanya recording kwa P-Funk kwasababu sasa hivi mimi nina studio yangu mwenyewe binafsi nikiwa na ndugu zangu Wanaume Halisi. Kiprofessionally P-Funk anatisha,” alisema.

Amesema tayari kuna wimbo wa kushirikisjwa atafanya kwa Majani ambapo Jay Mo na Mchizi Mox nao watakuwemo.

Katika hatua nyingine, Nature amesema yeye ni msanii mkubwa na anaweza kufananishwa na rappers kama KRS One, Mobb Deep au Nas.

“Huwezi kunifananisha mimi na Wiz Khalifa, Wiz Khalifa bwege tu,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents