Burudani

Kala Jeremiah aeleza kwanini mwaka huu hana mpango wa kuachia albamu

Msanii wa muziki wa hip hop Kala Jeremiah amefunguka kwa kusema kuwa mwaka huu hana mpango wa kuachia albamu mpya kutokana na kazi kubwa ambayo aliifanya katika albamu yake iliyopita.
Kala

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Kala amesema albamu yake iliyopita bado inaendelea kumpatia mshavu mpaka sasa.

“Kusema kweli kazi ambayo niliifanya kwenye albamu yangu iliyopita ilikuwa ni kubwa sana, albamu yangu ilikuwa na nyimbo 23,” alisema Kala. “Hata msanii ufanye vipi huwezi kuachia nyimbo 23 ndani ya mwaka mmoja hata miwili kama ukiamua kuachia wimbo mmoja mmoja, kwa hiyo mimi najua bado albamu yangu ina muda wakutosha kwa wananchi, mwaka huu sina mgango wa kuachia albamu,”

Rapa huyo alisema albamu hiyo bado inaendelea kumpatia mashavu mbalimbali katika muziki wake kwa kuwa hiyo ni CV ambayo anatembea nayo katika maisha yake ya muziki.

Kala kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Wanandoto’ ambao aliutoka miezi miwili iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents