Habari

Kampeni ya ‘Nipe Fagio Taka Taka Bucket Challenge’ kuanza Dar

Kampeni inayojihusisha na uhamasishaji usafi jijini Dar es Salaam ya ‘Nipe Fagio’ imeanzisha kampeni nyingine iitwayo ‘Nipe Fagio Taka Taka Bucket Challenge’.

10898205_504147043058224_4864611066646178411_n

Katika kampeni hiyo watu watakuwa wakitakiwa kuchukua ndoo au vyombo vya kuwekea uchafu ambavyo huvijaza takataka na kumtaja rafiki au mtu wake wa karibu kufanya hivyo pia.

Kampeni hiyo itakuwa ikifanyika kupita mitandao ya Instagram na Facebook.

“Eneo la kukusanya taka hizo linaweza kuwa popote pale aidha mtaani kwako, mtaa unaofanya kazi au mtaa unaopendelea kwenda,” yanasema maelezo ya kampeni hiyo.

Tayari wasanii kadhaa wamejitolea kushiriki pia kwenye kampeni hiyo.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents