Habari

Kamusi itasaidia Watanzania kujua Kiswahili kwa fasaha – Mama Salma Kikwete

Balozi wa Lugha ya Kiswahili na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete amewaasa Watanzania watumie kamusi ambayo imezinduliwa ili kuweza kutumia maneno sahihi na fasaha.

Mama Salma ameyazungumza hayo jana, mara baada ya uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

“Kiswahili kikitumika ndani ya bara letu la Afrika kila mtu atajivunia kuwa na lugha hii na ni fahari yetu sisi kama Waafrika kuwa na Lugha yetu ambayo ni ya Kiswahili kwani kila mwanadam ana kitu chake cha asili ambacho mwenyezi Mungu amemjaalia kuwa nacho, na sisi kama Watanzania lakini kama Waafrika ndio tunayo lugha hiyo ambayo ni ya Kiswahili kwahiyo uzinduzi wa Kamusi ya leo(jana) utasaidia na utachangia sana watu kuweza kujua Kiswahili,” alisema Mama Salma.

“Kutumia Kiswahili kwa matumizi yaliyokuwa sahihi na matumizi yaliyo fasaha, tunawashauri Watanzania wote watumie hii kamusi ambayo leo imefunguliwa ili kuweza kutumia maneno sahihi kwenye maneno stahiki, shime Watanzania tutumie Kiswahili kwa maendeleo yetu Watanzania.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents