Burudani

Kanye West abadili jina, adai Marekani ya Trump imekuwa mkombozi kwa vijana

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Kanye West ameamua kubadilisha jina hilo na kujiita YE, huku akishindwa kutoa sababu za kufanya hivyo.

https://twitter.com/kanyewest/status/1046064289944080388

Kwa upande mwingine, Kanye West amesema kuwa Marekani ya sasa inayoongozwa na Rais Donald Trump imejenga viwanda na kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.

“Kofia hii inaashilia kuwa hali ni shwari na Marekani inaenda pazuri. Hatutahitaji tena kutegemea mataifa mengine, tumejenga viwanda ili kuongeza ajira. Na tupo mbioni kufanya marekebisho madogo ya katiba kuwa kila mtu anayetoka jela apate ajira, Ujumbe umewafikia na nawapenda,“ameandika Kanye West kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kanye West amekuwa akimpigia upatu Rais Trump kwa muda mrefu, ingawaje wafuasi wa Chama cha Democratic ambao wengi ni jamii ya watu weusi wamekuwa wakimpinga na kumuita msaliti.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents