Habari

Mbosso afunguka mwanzo mwisho juu ya ukaribu wake na Esma Platnumz

Mbosso afunguka mwanzo mwisho juu ya ukaribu wake na Esma Platnumz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyoko chini ya lebo ya WCB Wasafi Mbosso Khan amefunguka juu ya ukaribu wake na dada yake na boss wake Diamond Platnumz ambaye ni Esma. Mbosso amesema Esma ni mshikaji wake sana na huwa wanaimba wote baadhi yimbo na mara nyingi humfundisha kuimba pia hufikia kipindi hadi anamshawishi na yeye aweze kuimba yaani ajiingize kwenye mambo ya muziki.

Mbali na kuongelea ukaribu wake na Esma lakini pia amekanusha vikali taarifa zilizokuwa zinasema kuwa yeye ana mahusiano na dada mwingine wa Diamond ambaye pia ni msanii Queen darlin,na kusema hama mahusiano nae kabisa.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents