Habari

Mwimbaji Mbasha asikitishwa na taarifa iliyotolewa na Bodi ya nyama

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabishara mkubwa nchini Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa iliyotolewa na Bodi ya Nyama juu ya Mfungaji wa Nguruwe kutokea Bahi Mkoani Dodoma Maarufu Kama Mr. Manguruwe.

Mbasha amesema aliona Mitandaoni taarifa ya Bodi ya Nyama wakisema kuwa Mfungaji huyo amekiuka sheria kwani alipewa kibali cha kufuga Nguruwe 49 tu, na sasa ana Nguruwe zaidi ya 1, 000, amesema kwanza Mfungaji huyo anapaswa kupongezwa na ni kitu ambacho haiwezekani kubakia na idadi hiyo kwani Nguruwe hao wanazaliana kila siku.

Aidha, amesema haoni sababu ya Bodi hiyo kuongea mambo hayo Mitandaoni bali wangemuita mdau wao/muwekezaji huyo na kuongea naye kiofisi na kumshauri cha kufanya ili wasimvunje Moyo bali wampe ushirikiano ili kukuza sekta ya Uwekezaji na Ufugaji kwa ujumla.

Mbasha amefunga Safari kutoka Jijini Dar es Salaam hadi Dodoma kwa ajili ya kujionea mradi huo wa Nguruwe, na kukili kuwa iwapo muwekezaji huyo atapewa ushirikiano basi ataikuza sekta ya Uwekezaji, Mifugo na Biashara kwa ujumla ambayo ndio maono Ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mifugo Mhe. Abdallah Ulega.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents