Habari

IGP Wambura awavalisha Nishani Maafisa wa vyeo mbalimbali wa Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amewavalisha Nishani Maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Mikoa ya Kanda ya kaskazini ikihusisha Mkoa wa Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro Mei 22,2024.

Nishani hizo walipewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.

IAmbapo jumla ya maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 630 wametunikiwa nishani za Nishani ya kumbukumbu ya Mungano,Nishani ya Utumishi uliotukuka,Nishani ya Utumishi wa Muda mrefu ,Nishani ya utumishi Mrefu na Tabia njema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents