Burudani

Kendrick Lamar ampiku Drake kwa mauzo

Rapa tokea Marekani Kendrick Lamar amevunja rekodi ya mauzo ya “Damn” kwa kumpita Drake ndani ya wiki moja.

Album hii ya ”Damn” imeuza kopi laki 603,000 katika wiki yake ya kwanza na kuwa album yenye mauzo makubwa huku ikifunika album ya Drake “More Life”, iliyouza kopi 505,000 kwa wiki yake ya kwanza.

‘Damn’ imekua Album yenye mauzo makubwa kwenye maisha ya muziki wa Kendrick Lamar. Awali album yake ya ‘Pimp a Butterfly’ iliuza kopi 324,000 kwa wiki ya kwanza.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents