Habari

Kila kitu kinawezekana hapa hapa Bongo – Rama Dee

Msanii wa R&B, Rama Dee ambaye kwa sasa anaishi na kufanya shughuli zake nchini Australia, amezungumzia tofauti iliyopo katika ufanyaji muziki Tanzania na ughaibuni.

12328510_1276263192402809_1448689995_n

Akiongea na BBC Swahili, Rama Dee alisema, “Unajua huku kwetu sasa hivi wasanii wengi wanaenda kwa miongozo ya mameneja na unakuta basi lazima upate skendo wenyewe wanaita kiki ili upate kuendelea mbele hivi vitu mie sijaviona huku Australia huku naona kama unafanya muziki wa Hip Hop kuna upande wa watu wanakusapoti na kama unafanya muziki wa R&B au Country pia ni hivyo hivyo kuna wanaosapoti na mashabiki wapo kabisa. Kitu kama kama hiki hapa Tanzania sikioni.”

Kuhusu mtindo wa wasanii kwenda kufanya video nje ya nchi, muimbaji huyo alisema:
“Kuna watu wanaweza kutengeneza hapa hapa kwetu mimi huwa siamini kuhusu Afrika Kusini au wapi kama una idea nzuri na kamera nzuri na mka share idea na director na mkafanya kitu kizuri kabisa hapa hapa.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents