Michezo

Kiungo wa Manchester United McTominay “Kwangu Mourinho atabaki kuwa special, nina deni kubwa sana kwake” – Video

Kiungo wa Manchester United McTominay "Kwangu Mourinho atabaki kuwa special, nina deni kubwa sana kwake" - Video

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Scotland Scott McTominay amefunguka mengi na kumtupia sifa nyingi aliyewahi kuwa kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho na kusema “Jose Mourinho anashika na kukaa sehemu maalum sana moyoni mwangu” na kufafanua kwamba bado anaendelea kuwasiliana naye.

Ikumbukwe Mourinho alimpa nafasi McTominay ya kuitumikia United, na kumfanya kiungo huyo kucheza kwenye mechi ya Ligi ya Premia Arsenal mnamo mwaka 2017.

McTominay, ambaye alitumiwa katika majukumu mengi tofauti na Mreno, ameendelea kuwa muhimu uwanjani kitu ambacho ni matunda ya Mourinho na hadi hivi sasa meneja mpya  Ole Gunnar Solskjaer anaendelea kumtumia kwa asilimia kubwa United.

Licha ya Mourinho kuondoka United, Mourinho bado ana uhusiano mzuri na McTominay – mchezaji huyo alisema “daima atakuwa rafiki yangu” na anaendelea kuwa na ushawishi katika kazi yake.

“Jose ni muhimu sana kwangu,” McTominay aliwaambia Sky Sports News. “Bado anaendelea kuwasiliana nami sasa na anaendelea kuwasiliana baada ya michezo kadhaa.

“Daima ataendelea kuwa na sehemu maalum ndani yangu na katika mioyo wa familia yangu kwa sababu ndiye aliyenileta, ndiye aliyeniamini.”Nina deni kubwa kwake kwa sababu ikiwa nisingekuwa kwake mimi labda nisingekuwa hapa sasa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents