Burudani
Kizz Daniel awakataa Wanigeria
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2024/03/Screen-Shot-2024-03-20-at-13.59.37.png)
Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Kizz Daniel ameamua kuwatolea uvivu wanaosema kuwa mkewe ni mbaya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram upande wa Komenti Kizz amekuwa akiwajibu mashabiki hao wanaojadili muonekano wa mkewe Oliwatobiloba Daniel.
Maneno hayo yamekuja baada ya Kizz Daniel kumpost mkewe kwenye Kurasa zake za Mitandao ya kijamii na kutangaza kuwa amemuoa miaka minne iliyopita na hivyo wasahau kama atamuacha.
Imeandikwa na Mbanga B.