Burudani

Komasava ya Diamond yagusa zaidi ya Mataifa 70 Duniani

Kwenye ngoma mpya ya Diamond Platnumz KOMASAVA amejaribu kufanya wimbo ambao utagusa mataifa mengi kwa namna wanavyosalimiana.

Kwenye wimbo mmoja kuna salamu za mataifa zaidi ya 10 ambayo ni Kiswahili kinachozungumzwa na mataifa zaidi ya matatu Kiingereza mataifa zaidi ya 10, Kifaransa Mataifa zaidi ya 10, Kireno zaidi ya Mataifa 7, Kichina ambacho kinazungumza zaidi ya watu bilioni 2 duniani kote, Kiarabu zaidi ya mataifa 10 na lugha zingine.

Wimbo huu utakuwa rahisi kusikilizwa kwenye mataifa mengi kutokana na kuwagusa kwa lugea zaidi.

Faida yake ni kwamba wimbo huu unaweza kwenda mbali zaidi kutokana na mataifa mengi  kuelewa kinachozungumzwa kwenye wimbo husika.

Vitu vinavyosaidia wimbo kuwa hit ni Ubora wa wimbo, kupitia mashairi, Melody ya wimbo husika, Beat ya wimbo husika na mengine.

Diamond aliwaza mbali kibiashara na pia wimbo kwenda mbali zaidi Kimataifa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents