Habari

Korea Kaskazini yafanya jaribio lingine la kombora, Yadai sasa inaweza kuipiga Marekani popote

Korea Kaskazini imefanya jaribio lingine kubwa la makombora ya nyuklia ya mafasa marefu ambapo imesema kuwa Makombora hayo yanauwezo wa kufika eneo lolote nchini Marekani.

Tokeo la picha la kim jung un
Rais Kim Jung-un

Taarifa zilizotolewa jana na runinga ya taifa hilo KCTv,  zimesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu zaidi kinyuklia duniani.

Kombora hilo lililopewa jina la Hwasong-15 ambalo Korea Kaskazini imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa zaidi duniani lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano wiki iliyopita.

Soma na hii – Trump amuonya Rais wa Korea Kaskazini kuhusu makombora ‘usitujaribu’

Mamlaka ya mawasiliano nchini humo (KCNA) kimesema kuwa kombora hilo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53.

Kombora hilo lililofyatuliwa kwa mwinuko halikupitia katika anga ya Japan kama makombora mengine hapo awali na lilianguka kilomita 250 karibu na pwani yake ya kaskazini , kulingana na maafisa wa Japan.

Soma zaidi–>Marekani yarusha ndege za kivita Korea Kaskazini kuonesha ubabe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents