Habari

Picha: Mama Wema Sepetu atua Nairobi kumuona Mhe. Tundu Lissu

Mama Mzazi wa msanii wa filamu Bongo na Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu wameenda Nairobi nchini Kenya kumjulia hali mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu ambaye anapata matibabu nchini huyo.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa akitibiwa Nairobi tangu aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi September mwaka huu. Viongozi mbali mbali wa kiserikali na wa chama hicho wamekuwa wakienda kumjulia hali na sasa Mama wa Wema Sepetu ameonekana kufanya hivyo.

Hapo jana Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluu alimtembelea pia Lissu hospitalini hapo. Utakumbuka Mama Wema pamoja na wanaye February 24 mwaka huu walitangaza kujiunga na Chadema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents