Burudani

Kunani kati ya Ben Pol na Alikiba? Tweets hizi zazusha utata mkubwa!

Kuna tatizo kati ya Ben Pol na Alikiba?

Kiba

Au Ben ameamua kutoa mtazamo wake wa moyoni juu ya hitmaker huyo wa Chekecha? Maswali ni mengi lakini ukweli ni kwamba tweet ya Ben kwa Kiba ina utata mkubwa.

“Bro @OfficialAliKiba mi naona kama unakuwa overrated halafu inakugharimu.. au Haikugharimu?” ameandika Ben Pol.

Well, neno ‘overrated’ ndio kiini cha ujumbe wa Ben Pizze ambalo wabongo wengi wamelitafsiri kivyao!

Kwa mujibu wa kamusi Cambridge ‘Overrate’ ni: If something or someone is overrated, that person or thing is considered to be better or more important than they really are.”

Tafsiri yake ni kuwa: Kama kitu au mtu akiwa overrated, kitu hicho au mtu huyo anafikiriwa ni bora au wa muhimu zaidi kuliko walivyo. Kwa maana nyingine ni kuwa mtu akiwa overrated ni kuwa anakuzwa wakati hana lolote!

Kwanini Ben Pol amesema hivyo? Tunafanya jitihada za kumpata afafanue lakini Alikiba amemjibu.

“InshaALLAH Kheri @IamBenPol Asante kwa kunyoosha Kidole sio makosa yako Ni dua inafanya kazi yake #KingKiba.”

Una mtazamo gani? Shusha comments zako hapo chini..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents