Habari

Kushinda urais Marekani unahitaji kura 270 

Mpaka muda huu ni vugumu kutabiri ni nani kati ya Donald Trump au Joe Biden atakuwa Rais wa taifa la Marekani kufuatia kura zinazoendelea kuhesabiwa.

Ili kuwa Rais wa Marekani mgombea lazima ashinde angalau jumla ya kura 270 ya wajumbe ambapo kila Jimbo lina kura ya wajumbe kulingana na idadi ya watu.

Kwa ujumla kuna kura 538 za majimbo na yule atakayepata angalau 270 ndio anakuwa Rais wa taifa la Marekani. Kwahiyo ikiwa utashinda jimbo, unashinda na kura yake isipokuwa kwa maeneo ya Nebraska na Maine lakini kidogo hilo linakanganya.

Itachukua siku kadhaa mpaka kupata matokeo ya urais Marekani kwa kuwa kura nyingi zilizopigwa kwa njia ya posta bado hazijahisabiwa katika baadhi ya majimbo.

Kuna zaidi ya kura milioni 1.4 zilizopigwa kwa njia ya posta ambazo bado hazijahesabiwa katika jimbo la Pennsylvania, na huenda ikachukua siku kadhaa kuzihesabu. Miji mikubwa ya Michigan (Detroit) na Wisconsin (Milwaukee) pia bado kura za eneo hilo hazijahesabiwa zote, na huenda zikaelekea kwa Democrats.

Kupata Updates za uchaguzi bofya HAPA

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents