Habari

Kutana na mtanzania aliyewashawishi majaji wa American Idol kumpa tiketi ya kwenda Hollywood

idol

Kijana aliyezaliwa na mama wa Kitanzania na baba wa Kikenya, Sanni M’mairura hivi karibuni aliwaacha hoi majaji wa shindano la American Idol 2013 kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kuimba na hivyo kuvuka hatua inayofuata.

Sanni ambaye aliulizwa na majaji kama anaweza kuongea lugha ya wazazi wake aliongea ‘Ndio naweza kuongea Kiswahili’ kwa kujiamini kabla ya kuanza kuimba wimbo wake. Baada ya kuimba majaji wote wanne ambao ni pamoja na Nick Minaj, Mariah Carey na Randy Jackson walikikubali kipaji chake na hivyo kumpa tiketi ya kwenda Hollywood ambako washiriki wote waliochaguliwa kutoka majiji mbalimbali nchini Marekani huwekwa kambini.

http://www.youtube.com/watch?v=VkbuLhM9R5s

Kabla ya kushiriki American Idol, Sanni amekuwa akifanya cover za nyimbo mbalimbali za wasanii akiwemo Justin Bieber na kuzipost Youtube. Huu ni mwanzo mzuri wa kijana huyo kuelekea kwenye usupastaa.

Mtazame hapa akifanya cover ya wimbo wa Justin Bieber

http://www.youtube.com/watch?v=b-4QjVvGmjc

Unaweza kumfollow Twitter kwa @SaNniMmairura.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents